Skip to content
Advertisements

Hizi ndizo klabu zenye mishahara mikubwa

KAMA ilivyoripotiwa na Gazeti la The Mail on Sunday, mzigo mkubwa wa mishahara, hesabu zake zimepigwa kulingana na kiasi klabu inachotumia kulipa wachezaji kwa wiki. 

Klabu za Ligi Kuu England, zimetawala zaidi katika 20-Bora kuliko klabu za ligi nyingine, hivyo hebu tutazame ni timu gani zimo katika orodha hii… 
1. Barcelona- Pauni milioni 6.6 kwa wikiIkiwa na wastani wa mshahara kiasi cha pauni 126,875 kwa wiki, Barcelona ndiyo timu inayolipa zaidi na taarifa za hivi karibuni za Leo Messi kusaini mkataba mpya, kumeilazimisha miamba hiyo ya Catalunya kumlipa zaidi nyota huyo. 
2. Paris Saint-Germain- Pauni milioni 6.5 kwa wikiWameingia kwa kasi katika 10-Bora, hiyo ni kufuatia Neymar na Kylian Mbappe kutua PSG katika majira ya joto, na kuifanya klabu hiyo ya Paris kuwa miongoni mwa klabu zenye nguvu Ulaya. 
3. Real Madrid-Pauni milioni 6.2 kwa wikiImepaa zaidi kutoka nafasi iliyokuwapo msimu uliopita, mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga wamekuwa na mishahara mikubwa kila wiki.Hiyo ni kutokana na wanaoingiza kiasi kikubwa kama Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos na Gareth Bale. 
4. Manchester United- Pauni milioni 5.2 kwa wiki  
Mashetani Wekundu hawa, kwa ujumla wameporomoka kwa nafasi tatu tangu mwaka jana, kutokana na matokeo ya kuondoka kwa Wayne Rooney na Bastian Schweinsteiger.Lakini bado wanamajina makubwa ambao wanaipa nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, lakini wakiifanya kuwa moja ya timu inayolipa zaidi England. 
5. Manchester City- Pauni milioni 5.2 kwa wiki Imewafuata ‘Bavarian’ hao katika tano bora, Manchester City, kutokana na kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kwa sasa huku wengine wakiwa hawatumiki, jambo ambalo linaifanya pauni milioni tano kwa wiki zisitoshe kuwalipa. 6. Bayern Munich- Pauni milioni 5.2 kwa wikiKama ilivyo kwa Juventus Serie A, Bayern Munich nayo imekuwa ikitawala Bundesliga katika kila idara ikiwa ni pamoja na uwezo mkubwa wa kulipa mishahara.Hilo limeiwezesha kuwang’oa wachezaji kama Robert Lewandowski, Niklas Sule na Mats Hummels kutoka kwa wapinzani wao wakuu, Dortmund. 
7. Juventus- Pauni milioni 4.8 kwa wikiKwa mbali ndiyo timu tajiri zaidi Italia, ingawa inakaribia kufikia pengo lililopo kutoka klabu zote za Milan, wakongwe hao wanahakikisha wachezaji wote wanaocheza Turin inafanya makubaliano mazuri kama ilivyo kwa Paulo Dybala na Gonzalo Higuain. 
8. Chelsea- Pauni milioni 4.4 kwa wikiTangu Roman Abramovich, alipotua Magharibi mwa London, ‘The Blues’ haijawahi kuona shida kulipa nyota wanaowataka kiasi kikubwa cha mshahara na hilo linaifanya klabu hiyo ya Stamford Bridge kubaki kuwa klabu inayotumia fedha nyingi za usajili Ulaya. 
9. Arsenal- Pauni milioni nne kwa wikiMashabiki wa Arsenal ukweli watakuwa wakitegemea mzigo wa mishahara kuongezeka zaidi mwaka ujao kama watakuwa wamefanikiwa kuwaongeza mikataba nyota wao wawili Mesut Ozil na Alexis Sanchez.Hilo likitokea ni wazi wachezaji hao watataka kulipwa dau kubwa zaidi jambo litakaloifanya klabu hiyo kupaa kutoka katika nafasi hii ya sasa. 
10. Atletico Madrid- Pauni milioni 3.8 kwa wikiImetinga 10-Bora ya walipaji mishahara mikubwa kwa wiki, mwaka huu, ikiwa imepaa kwa nafasi tatu kwa kuipiku Liverpool na Spurs.Kupaa kwa mishahara Atletico Madrid, kumeongezeka kutokana na kuendelea kuwashikilia wachezaji kama Antoine Griezmann, Saul Niguez na Koke. 
Nafasi ya 11 hadi 2011. Liverpool – Pauni milioni 3.6 kwa wiki12. Tottenham Hotspur – Pauni milioni 3.1 kwa wiki13. AC Milan – Pauni milioni 3.1 kwa wiki14. West Ham – Pauni milioni 2.8 kwa wiki15. Everton – Pauni milioni 2.816. Borussia Dortmund – Pauni milioni 2.7 kwa wiki17. Inter Milan – Pauni milioni 2.6 kwa wiki18. Roma – Pauni milioni 2.6 kwa wiki19. Leicester City – Pauni milioni 2.5 kwa wiki20. Valencia – Pauni milioni 2.4 kwa wiki.

Advertisements
%d bloggers like this: