Skip to content
Advertisements

Mwanafunzi aliyevaa hijab azuiwa kufuzu chuoni Nigeria

Mwanafunzi wa sheria nchini Nigeria amazuiwa kufuzu baada ya yeye kusisitiza kuvaa hijab wakati wa sherehe za kufuzu.
Amasa Firdaus, ambaye alifuzu kutoka chuo cha Ilorin, alizuiwa kuingia ukumbi wa kufuzu kwenye mji mkuu Abuja ambapo sherehe zilikuwa zikifanyika.
Alikataa kuvua hijab yake akisitiza kuwa angevaa kofia ya kufuzu juu ya hijab yake.

Hii ilitajwa kuwa kuenda kinyume na vazi ramsi lililoweka na vyuo vya sheria.
Kesi hiyo imevutia husia kubwa katika mitandao ya kijamii.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alisema kuwa Bi Firdaus ana haki ya kufanya hivyo.

Advertisements
%d bloggers like this: