Skip to content
Advertisements

Zanzibar Heroes yapokelewa kifalme

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayubu Mohamed Mahmoud ameongoza maelfu ya wazanzibar kuipokea timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ iliyotoka Kenya kwenye mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup yaliyomalizika jana.


Katibu mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo , Omary Hassani Kingi amewapongeza wachezaji walioiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano hayo.
“Vijana wameonesha mpira wa hali ya juu na pia kubwa wameonesha nidhamu ya hali ya juu katika michezo,nawashukuru wananchi wamejitokeza wengi sana, shamrashamra kuanzia jana walipokuwa wanaangalia mechi mpaka baada ya mechi na leo walivyojitokeza tumeonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuipenda timu yetu na vijana wetu ambao wamefanya kitu kikubwa.”

Kwa upande wa wachezaji, Hamad Mshamata amezungumzia changamoto ambazo walikutana nazo wakati wa safari yao kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano.
“Changamoto ilikuwa kwenye usafiri wakati wa kwenda, Kenya ni mbali sio karibu kama mtu anavyokwenda Arusha au Mwanza.”

“Wazanzibar wazidishe ushirikiano kama huu waliouonesha mwaka huu tangu timu inapoanza kuandaliwa kwa ajili ya mashindano yoyote. Ushirikiano ukianza mapema watu watakuwa na morali ya kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote tutakayokuwa tunashiriki kuliko kusubiri hadi tayari kitu kimeshatokea ndio wanaingia.”

Advertisements
%d bloggers like this: