Skip to content
Advertisements

Baadhi ya makada wa ANC kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani

     
Siku chache baada ya makamu wa rais Cyril Ramaphosa kuchaguliwa kuwa rais wa chama tawala cha ANC katika uchaguzi uliogubikwa na dosari, mwenyekiti wa majimbo ya Kaskazinin Magharibi Supra Mahumapelo amesema sintofahamu iliyogubika matokeo ya nafasi ya katibu mkuu huenda ikaishia mahakani.
Katika kinyang’anyiro kilichokuwa na upinzani mkali, nafasi ya katibu mkuu ilichukuliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa jimbo la Free State Ace Magashule aliyemshinda kwa kura chache tu mpinzani wake mwenyekiti wa jimbo la KwaZulu-Natal Senzo Mchunu.
Hata hivyo wafuasi wa Mchunu sasa wanapinga matokeo ya nafasi ya katibu mkuu wa chama, wakidai zaidi ya kura zaidi ya 68 hazikuhesabiwa.
Wakati suluhu ya sintofahamu hii ikisubiriwa, Mahumapelo anawatuhumu wale wanaopinga matokeo haya kuwa wana maslahi yao binafsi na kwamba mwisho wa siku watalazimika kwenda mahakamani.
Katika hatua nyingine rais mpya wa chama Cyril Ramaphosa amewataka wajumbe wa kongamano la 54 la chama hicho kuchagua wajumbe makini watakaoingia kwenye kamati kuu ya chama NEC.

Advertisements
%d bloggers like this: