Skip to content
Advertisements

Dina Marious Afunguka Mzazi Mwenzake

Mtangazaji maarufu Bongo, Dina Marious.

BAADA ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha mzazi mwenzake mtangazaji maarufu Bongo, Dina Marious, Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ akiwa anamchumbia mwanamke mwingine, mtangazaji huyo amefunguka kuwa, anabariki kwa mikono miwili ndoa hiyo.

Dina Marious akiwa na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ enzi za mahusiano yao.

Picha za Ruben akimvisha pete ya uchumba mwanamke mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, juzi Jumanne na kuzua gumzo ambapo watu wengi walikuwa ‘wakimtag’ Dina ili aweze kushuhudia. Waliokuwa wakikomenti katika mitandao ya kijamii, walionesha kusikitika na wengine kumuonea huruma Dina ambaye wametoka mbali na Ncha Kali kiasi cha kumzalia mtoto kisha kumuacha solemba. “Jamani mapenzi haya yasikieni hivi hivi.
 
Hivi unadhani Dina atakuwa anajisikiaje anapoona mwenzake anavalishwa pete na yeye waliyetoka mbali tangu wakiwa wanafanya kazi pamoja Clouds FM na sasa kila mtu ana maisha yake? Inauma kwa kweli,”alichangia mdau mmoja mtandaoni. Amani lilimvutia waya Dina ili kumsikia ana lipi la kuzungumza hususan baada ya picha hizo kusambaa mitandaoni na watu kumuonea huruma. “Mimi sina tatizo.
 
Huyo mtu tulishaachana ni zaidi ya miaka miwili sasa iliyopita, hivyo sioni jipya. Kwanza mimi binafsi sipendi hayo mambo ya mitandao kuweka mambo yangu binafsi. Ndio maana utaona mimi mara nyingi naposti kuhusu kazi basi,” alisema Dina ambaye sasa anakitumikia kituo cha Redio cha EFM. Jitihada za kumpata Ruben na mchumba wake mpya ili kuwasikia wanazungumziaje maisha yao mapya, hazikuzaa matunda kutokana na kutopatikana hewani.

Advertisements
%d bloggers like this: