Skip to content
Advertisements

Mwanajeshi mwingine wa Korea Kaskazini atorokea Korea Kusini

Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakitazama eneo la mpaka ambalo hivi karibuni mwenzao aliutumia kutorokea Korea Kusini. REUTERS/Kim Hong-Ji

Mwanajeshi wa Korea Kaskazini ametoroka nchi yake na kuingia Korea Kusini kupitia mpaka wenye ulinzi mkali unaozitenganisha nchi hizo, hatua iliyosababisha pande zote mbili kufyatua risasi.
Hili linakuwa ni tukio la pili mfululizo katika kipindi cha mwezi mmoja kwa mwanajeshi wa Korea Kaskazini kutoroka na kuingia Korea Kusini.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Korea Kusini amesema wanajeshi wake walimuona mwanajeshi huyo kwa kutumia vifaa maalumu akivuka mpaka na kukimbilia kwenye kituo cha ukaguzi cha wanajeshi wake.
Wakati mwanajeshi huyo akivuka hakukuwa na urushwaji wa risasi lakini dakika tisini baadae wanajeshi wa Korea Kusini walilazimika kufyatua risasi zaidi ya ishirini kuwaonya wenzao wa Korea Kaskazini waliokuwa wanasogelea eneo la mpaka kwa lengo la kumtafuta mwenzo.
Baadae ilisikika pia milio ya risasi kutokea Korea Kaskazini huku wizara ya ulinzi ikisema hakuna risasi iliyorushwa kuvuka mpaka wa nchi hizo.
Tukio hili linajiri ikiwa ni mwezi mmoja tangu kutokea tukio jingine kama hili la wanajeshi wa Korea Kaskazini waliotoroka kwa kutumia gari ambapo walijeruhiwa na wenzao waliokuwa wakiwafytaulia risasi kwenye mpaka wa Panmunjom.
Mwanajeshi aliyetoroka mwezi uliopita inaelezwa alilengwa na karibu risasi nne kabla ya kuokolewa na wanajeshi wa Korea Kusini na toka wakati huo amekuwa akipatiwa matibabu hospitalini.

Advertisements
%d bloggers like this: