Skip to content
Advertisements

NSAJIGWA KUWAPIKU MABOSI WAKE DHIDI YA MBAO FC

Baada ya kufungwa mara mbili na Mbao, sasa kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amekabidhiwa jukumu la kuikabili Mbao Jumapili

Klabu ya Yanga itaendelea kumkosa kocha wake mkuu George Lwandamina kwenye mchezo wa Jumapili ambao utachezwa uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza dhidi ya wenyeji Mbao FC.

Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa ameiambia Goal,

kocha huyo amefiwa na Mtoto wake na wamezika leo jioni hivyo hatoweza kuwepo kwenye mchezo huo na kocha msaidizi Shedrack Nsajigwa ataendelea kukiongoza kikosi chao kwenye mchezo huo.

“Nikweli kocha wetu yupo kwao Zambia, alipokwenda kuhudhuria mazishi ya Mtoto wake ambaye amezikwa leo jioni, hivyo kwa tukio hilo niwazi kwamba hatokuwa na timu Jumapili Jijini Mwanza badala yake atakuwepo msaidizi wake Nsajigwa ambaye ndiyo atakiongoza kikosi pamona na viongozi wengine wa benchi la ufundi,” amesema Mkwasa.

Kiongozi huyo amesema wanaimani kubwa na Nsajigwa, kwasababu ni kocha ambaye yupo na timu hiyo kwa muda mrefu na amekuwa akipata ujuzi kutoka kwa makocha tofauti waliokuwa juu yake hivyo wanaimani naye na watajitahidi kumpa sapoti ili waweze kushinda mchezo huo.

Nsajigwa ndiyo aliyeiongoza Yanga kushinda mabao 2-0, katika mchezo wa kufuzu hatua ya 32 bora wa kombe la FA, dhidi ya Reha FC, Jumapili iliyopita hivyo nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo na Taifa Stars, atahakikisha anapambana ili kushinda na kujijengea CV yake vizuri.

Advertisements
%d bloggers like this: