Skip to content
Advertisements

TRA wakesha katika baa, kumbi za starehe Moshi

Kwa wiki moja mfululizo, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamekuwa wakipiga kambi kwenye baa na kumbi maarufu mjini Moshi nyakati za usiku ili kuhakikisha wateja wanapewa risti za EFD.

Hii ni baada ya mji wa Moshi kujaa wageni wanaokuja na familia zao na kufanya manunuzi kwa wingi ili kusherehekea sikukuu mwishoni mwa mwaka.
Vyanzo kadhaa vimedokeza kuwa TRA imesukumwa kuchukua hatua hiyo kutokana na wingi wa wageni mkoani Kilimanjaro, ambao wamechangia kuongezeka kwa biashara.
Kwa wiki moja sasa mfululizo, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamekuwa wakipiga kambi kwenye baa na kumbi maarufu mjini Moshi nyakati za usiku.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa maofisa hao wamekuwa wakipiga kambi katika maeneo hayo ya starehe kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa stakabadhi za kielektroniki (EFD) kwa wateja.
Vyanzo kadhaa vimedokeza kuwa TRA imesukumwa kuchukua hatua hiyo kutokana na wingi wa wageni mkoani Kilimanjaro, ambao wamechangia kuongezeka kwa biashara.
Tangu Desemba 22 hadi jana, mji wa Moshi umefurika wageni kutokana na wenyeji wake kujenga utamaduni wa kurejea nyumbani kila mwisho wa mwaka kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya wakiwa na ndugu na jamaa zao.
Hali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara zote za kuingia na kutoka katika mji wa Moshi, huku maduka makubwa (supermarkets) na masoko yakielemewa na wateja.
Hata hivyo, Jumatatu idadi ya wageni ilionekana kupungua kutokana na wengi kwenda maeneo waliyozaliwa kusherehekea sikukuu. Maofisa wa TRA walionekana hadi usiku wa manane katika klabu na baa mashuhuri za Hugo Garden, Mekus Bristol, Red Stone, Pub Alberto, Kili Home na maeneo mengine ya biashara.
“Safari hii wamefanya kazi kama mchwa hakuna kulala. Mpaka usiku unakutana nao kwenye kumbi za starehe kuhakiki risiti. Mapato ya Desemba hii nafikiri yatavunja rekodi,” alisema mmoja wa watu waliowashuhudia maofisa hao.
Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo alisema lengo la hatua hiyo ni kuwakumbusha wafanyabiashara kutoa risiti za EFD.
“Unajua kuna wageni wengi wamekuja na maana yake kuna biashara kubwa inafanyika. Tuliona ni vyema tukatembelea maeneo hayo ili kuwakumbusha wajibu wao wa kutoa stakabadhi za kielektroniki,” alisema.
Mbibo alisema kazi hiyo haina maana kwamba kuna udanganyifu, bali kwa sababu kuna unywaji wa pombe na kupagawa kwa sababu za sikukuu, wahudumu wanaweza kupitiwa kutoa risiti za EFD.
Meneja huyo alisema kazi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na walipata ushirikiano kutoka vyombo vya ulinzi na usalama hususan Jeshi la Polisi na ofisi ya mkuu wa wilaya.

Advertisements
%d bloggers like this: