Skip to content
Advertisements

Young Dee Amponda Amber Lulu

MKALI wa ngoma ya KibenTen, David Genzi maarufu kwa jina la Young Dee, amemponda mpenzi wake wa zamani, Amber Lulu kuwa hana hadhi ya kuwa naye kwa sasa.

Akichonga na Risasi Vibes, Young Dee alisema kwa sasa yupo kwenye uhusiano ‘siriaz’ na mwanadada ambaye hayupo tayari kumuweka wazi, lakini siyo mama wa mtoto wake wala Amber Lulu.

Nimechoka kuulizwa maswali kuhusu kuwa kwenye uhusiano na Amber Lulu, hana hadhi ya kuwa na mimi na ninaomba nisiharibiwe uhusiano wangu na mpenzi wangu ambaye nipo naye kwa sasa,” alisema Young Dee.

Wawili hao wamejikuta katika malumbano kufuatia wiki iliyopita, msichana huyo kusema kuwa ni kumkosea heshima kumfananisha mpenzi wake wa sasa, rapa wa Kenya, Prezoo na kijana huyo wa Dar es Salaam.

Advertisements
%d bloggers like this: