Skip to content
Advertisements

Imetajwa sababu iliyomkimbiza Chirwa Yanga

Baada ya kuenea taarifa kwamba mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ameikimbia klabu hiyo na kurejea nyumbani kwao Zambia akishinikiza kulipwa fedha zake anazodai, uongozi wa wanajangwani umesema Chirwa amekwenda nyumbani kwa sababu za kifamilia.
Habari zinsema kwamba, Chirwa aliomba uongozi wa Yanga ummalizie fedha anazodai ndipo arejee nchini kujiunga na kikosi chao kwa ajili ya kuendelea kukitumikia.
“Obrey Chirwa alisafiri kwa matatizo ya kifamilia alikwenda Zambia, tunataraji anaweza kurejea wakati wowote kuanzia hivi sasa. Yapo maneno mengi yanazungumzwa kwenye mitandao ya kijamii lakini kama taasisi si kila jambo tunaweza kuliweka hadharani, mchezaji anapokuwa na tatizo la kifamilia basi klabu inasimama upande wake kuangalia namna ya kumsaidia hata kama yeye mwenye anapokuwa na matatizo na klabu kuna taratibu za kushughulikia matatizo hayo”-Dismas Ten afisa habari Yanga.
“Obrey Chirwa bado ni mchezaji wa Yanga na kama kutakuwa na taarifa nyingine basi zitatolewa baadaye lakini kwa sasa bado ni mchezaji wa Yanga na atakuwepo kwenye kikosi kwa mujibu wa mkataba wake mpaka pale utakapokuwa unakwenda kwenye hatua nyingine.
“Niwatoe wasiwasi wana Yanga, klabu imesajili wachezaji 29 wa kikosi cha juu na tumeongeza wachezaji wengine wawili ingawa bado hawawezi kutumika kwa sasa kwa sababu leseni hazijatolewa na kamati ya usajili ya TFF inaendelea kufanya taratibu zinazohitajika ili kuweza kukamilisha hadhi za wachezaji waliosajiliwa wakati wa dirisha dogo.”
Hivi karibuni Chirwa ali-post picha kwenye account yake ya Instagram akiwa shambani anapalili mahindi kwa jembe la mkono.

Advertisements
%d bloggers like this: