Skip to content
Advertisements

MAMA MENSEN AFIA MIKONONI MWA PAM D

MAMA mzazi wa mwanamuziki Mensen Selekta, siku ya Jumatatu, wakati watu wakisherehekea Sikukuu ya Krismasi alifariki majira ya saa kumi jioni kutokana na ugonjwa wa Kisukari.

Akizungumza na Showbiz-Xtra kwa majonzi Mensen alisema, mama yake aitwaye Lucy alianza kujihisi hali ya tofauti siku ya Jumapili, ambapo Jumatatu hali ilibadilika zaidi na walipompeleka hospitali aliweza kupoteza maisha.

“Nimeumia sana, mama yangu amefariki hospitali akiwa mikononi mwa binamu yangu Pam D, tunategemea kusafirisha siku ya Alhamisi, kwenda Tanga kwa ajili ya maziko,” alisema Mensen, ambapo Pam alipotafutwa alisema shangazi yake dakika za mwisho kifua kilimbana sana akakosa pumzi na kumsababishia umauti.

Advertisements
%d bloggers like this: