Skip to content
Advertisements

MOBETO: HUYU ZARI ATAMUUA MAMA YANGU

DAR ES SALAAM: Wamefika pabaya! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia bifu kubwa kufukuta kwenye familia ya mwanamitindo, Hamisa Mobeto na mfanyabiashara, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Bifu hilo limeshika kasi kufuatia warembo hao, kila mmoja kuzaa na msanii mmoja wa Bongo Fleva ambapo safari hii, Mobeto ameibuka na kusema, Zari anaweza kusababisha kifo cha mama yake mzazi.


TUANZE NA CHANZO

Kabla Mobeto hajafunguka, chanzo kilicho karibu na mrembo huyo, kiliweka bayana kuwa, bifu la Mobeto na Zari limefikia pabaya hususan baada ya kuwahusisha hadi wazazi jambo ambalo linaweza kuleta maafa.

“Unajua wamefika pabaya. Wafuasi wa Zari mitandaoni wanamuandika vibaya sana mama Mobeto. Imefika mahali hadi mama Mobeto anapandwa na presha. Watamuua mama wa watu jamani.

 

ATAJA KINACHOMPOZA MOBETO

“Unajua tatizo ni kwamba, Mobeto hana mashabiki wengi katika ukurasa wa Instagram kama alivyo Zari. Zari ana wafuasi zaidi ya milioni 3 na nusu wakati Mobeto ana milioni 1 na laki 9 hivyo ni dhahiri Team Zari wakiamua kumpa za chembe Mobeto, lazima akae,” kilisema chanzo hicho.

MOBETO HUYU HAPA

Baada ya chanzo hicho kuweka nukta, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mobeto na kumuuliza kuhusu bifu hilo kufikia kwenye hatua mbaya ambayo inaweza kumsababishia matatizo mama yake ambapo alifunguka.

“Yani kwa kweli Zari huyu atamuua mama yangu. Unajua nini, hawa watu wanaompigania Zari katika mitandao ya kijamii, kwa sasa wamefikia hatua mbaya sana.

 

“Wanamtukana sana mama yangu bila hata sababu za msingi. Yani kuna vitu vizito sana vinaandikwa hadi mama anapata mshtuko,” alisema Mobeto.

 

Mrembo huyo aliweka wazi kuwa, endapo Zari angewasihi watu wake waache kumtukana mama yake, wangeweza kumtii lakini kwa sababu amekaa kimya, ndio maana wanapata kichwa.

 

ASHAURIWA MAMBO YA KUFANYA

Shosti wa Mobeto ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, alimshauri mrembo huyo kufanya mambo matatu ya msingi ambayo yatamfanya awe salama, yeye pamoja na mama yake.

 

JAMBO LA KWANZA

“Aache kushindana na Zari. Yeye asifanye kitu kwa kushindana na Zari. Afanye kazi zake bila kuonesha kwamba anamtambia Zari au kutaka kushindana naye kwa namna yoyote.

“Si unakumbuka alivyoandaa shughuli ya arobaini ya mwanaye, yani aliweka zile mbwembwe za gharama ili mradi tu afikie levo za Zari kitu ambacho si sahihi. Alijikuta anaahirisha shughuli hiyo kwa kukosa fedha hadi pale alipofanikiwa ndio ikafanyika.

“We angalia shoo ya juzi kule Uganda, kakubali kwenda kufanya shoo siku moja na Zari bila kujua kule mwenzake ni kwao hivyo kujikuta akifunikwa bila sababu za msingi.”

 

JAMBO LA PILI

“Ili awe salama, hapaswi kujibu wala kuanzisha kijembe chochote katika mitandao ya kijamii. Yeye aweke masuala yake yanayomhusu tu, aachane kabisa na Zari.”

 

JAMBO LA TATU

“Akae mbali na mzazi mwenzake ambaye anaonekana kulalia kwa Zari. Ni dhahiri kwamba mwenzake ndiye kinara katika huu mvutano. Zari amekaa muda mrefu kwenye uhusiano kuliko yeye hivyo hawezi kumuacha kirahisi. Yeye angetafuta tu mwingine, akaendelea na maisha yake,” alimaliza rafiki huyo wa Mobeto.

 

TUJIKUMBUSHE

Miezi kadhaa iliyopita, Mobeto aliingia kwenye uhasama mkubwa na Zari baada ya kubainika kuwa amezaa na msanii wa Bongo Fleva ambaye alikuwa kwenye uchumba wa muda mrefu na Zari.

Uhasama huo ulikolea zaidi baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa, Mobeto alijiingiza kwenye uhusiano wa siri na jamaa huyo wa Zari kiasi cha kulala katika kitanda chake, anacholala pindi anapokuwa nchini.

Baada ya bifu hilo kupamba moto kwenye mitandao ya kijamii, juzikati lilihamia kwa wazazi baada ya mama mkwe wa Zari, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuolewa na kijana mdogo (benteni) kisha mama Mobeto kudaiwa kumkejeli Sandra mitandaoni na kusababisha wazazi hao nao waanze kutukanwa mitandaoni.

Advertisements
%d bloggers like this: