Skip to content
Advertisements

Mtoto wa Lwandamina alijiua baada ya kubaka 

Inaelezwa kwamba mtoto wa kocha wa Yanga George Lwandamina anaefahamika kwa jina la Mofya amejiua baada ya kujaribu kumuua mwanamke mwenye miaka 25.
Mofya, 28, mkazi wa eneo la Water Works lililopo Libala Township, akiwa pamoja na Keith Chemu, 16, mkazi wa eneo hilo pia wanadaiwa kumkaba, kumpiga na kumbaka mwanamke huyo ambaye alikutwa na majeraha kadhaa sehemu za shingo na kifuani.
Msemaji wa jeshi la polisi Esther Katongo amesema, shambulio kwa mwanadada huyo limetokea Ijumaa ya juma lililopita majira ya saa 8:00 mchana kwa saa za Zambia huku watuhumiwa wakiiba kiasi cha pesa pamoja na simu ya mkononi aina ya Sumsung mali ya mlalamikaji.
Bi. Katongo amesema, Mofya alijiua kwa kunywa sumu wakati Keith yeye akiwa mikononi mwa jeshi la polisi. Alisema mwathirika wa tukio hilo alikuwa anaendelea kutibiwa kwenye hospitali ya University Teaching Hospitals (UTH) jijini Lusaka.
George Lwandamina wakati akifanyiwa mahojiano alithibitisha kwamba, Mofya ni kijana wake, inaelezwa kuwa, hadi umauti unamkuta Mofya alikuwa akifanya mazoezi na FAZ inayoshiriki ligi kuu ya Zambia.
Chanzo: Times of Zambia

Advertisements
%d bloggers like this: