Skip to content
Advertisements

NISHA BWANA’KE WATUPIANA VIJEMBE!

STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye siku chache zilizopita alikana kuachana na mwandani wake Minu, amejikuta akikumbwa na aibu baada ya kuandika ujumbe ulioashiria kuwa, uhusiano wao umevunjika na kisha mwanaume huyo kujibu mapigo.

 

Kupitia ukurasa wake wa kijamii, Nisha aliandika ujumbe mrefu ulioonyesha kukerwa na kitendo cha kuibiwa mabwana zake wawili na kuhitimisha kuwa mpenzi wake wa sasa hatomuanika, jambo lililomchefua Minu ambaye naye alijibu mapigo kwa kusema kuwa; “Mwanamke akimwaga mboga, usimwage ugali chukua tambara upige deki.”

 

Kutokana na vijembe hivyo paparazi wetu alimvutia waya Nisha ambaye aliishia kucheka na kusema kuwa; “Jamani kwani hapo nimesema nimepata mwingine hahaa,”alisema mwanadada huyo, huku jitihada za kumpata Minu zikigonga mwamba, simu yake haikupatikana hewani

Advertisements
%d bloggers like this: