Skip to content
Advertisements

Pretty Kind afunguka kufanyishwa ngono

Msanii wa muziki na filamu Suzan Michael maarufu kama ‘Pretty Kind’, ambaye alishawahi kupelekwa nchini India na marafiki na kwenda kufanyishwa biashara ya ngongo, atoa siri ya watu wengi waliopo huko na hofu yao ya kurudi nyumbani.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Pretty Kind amesema maisha wanayoishi wasichana wanaotoka huku na kwenda kule ni magumu, kiasi kwamba wanahofia hata kurudi nyumbani kwni hawana kitu chochote wala fedha.

Pretty Kind ameendelea kueleza kuwa maisha ya biashara ya ngono yanawapa wakati mgumu kwani kuna muda wanashindwa hata kula pamoja na kupatwa na misuko suko mingine, lakini wanaona aibu kuja kuzikabili familia zao baada ya kuziacha kwa muda mrefu.

“Unajua mi nilivyochukulia mara ya kwanza yatakuwa ni maisha kama tunavyoishi bongo, nilienda kule niliitwa na msichana mwenzangu akaniambia nitapata kazi ya hela nyingi, nilipofika nikashangaa, watu niliowakuta kule maisha magumu, wanatamani kurudi nyumbani lakini wanaona aibu, anatrudije nyumbani hana kitu cha maana, na familia inajua yuko nje, na kwanza muda mwengine unakuwa ushanyang’anywa passport unalipa madeni ya watu”, amesema msichana huyo ambaye kwa sasa amegeukia bongo fleva.

Pretty Kind hivi sasa ana kazi mpya ya bongo fleva inayoitwa ‘Vidudu washa’ aliyomshirikisha Gigy Money, baada ya kujaribu kwenye filamu nakuona hailipi.

Advertisements
%d bloggers like this: