Skip to content
Advertisements

Jennifer wa Kanumba Akacha Kuigiza

MSANII ‘mtoto’ katika tasnia ya uigizaji nchini, Hanifa Daudi ‘Jennifer’ amesema hana mpango wa kuifanya kazi ya uigizaji kama tegemeo la kujikimu kimaisha na ndiyo maana kwa sasa ameamua kujikita kikamilifu katika masomo.

Katika kubadilishana mawazo na Star Mix, Jennifer ambaye umaarufu wake ulichomoza kupitia Filamu za This Is It, Uncle JJ na nyinginezo ambazo alishiriki na marehemu Kanumba, alisema masomo yamekuwa magumu hivyo kumchukulia muda mwingi lakini pia amegundua kutokuwa na wito kwenye sanaa ya uigizaji na badala yake ni bora kufukuzia ndoto zake za kimaisha.

 

“Kwa kweli sina mpango wa kuwa muigizaji katika maisha yangu, masomo yamechukua sehemu kubwa ya muda wangu, kwa sasa niko nyumbani kwa ajili ya likizo labda kama ikitokea kuna kazi ya filamu naweza kufanya lakini siyo kwamba eti iko akilini mwangu kama sehemu ya maisha yangu, hapana kwa kweli,” alisema Jennifer.

Advertisements
%d bloggers like this: