Skip to content
Advertisements

Mjue Alek Wek Model mwenye heshima kubwa duniani.

Alek Wek

Supermodel Alek Wek(40) mwenye heshima kubwa ulimwenguni. Alek amefanya kazi na fashion brand zote kubwa za kifahari duniani. Ni mwanamitindo wa daraja A miaka ya 1990s na 2000s, kwa miaka mingi sasa amekuwa cover girl kwenye majarida maarufu nchi nyingi Ulaya na Marekani yakiwemo Elle, Cosmopolitan, Glamour

.

Alek ambaye alianza modelling 1995 mwaka uliofuata alitokea katika video ya Janeth Jackson “Got til it’s gone” mwaka 1997 akawa mshindi wa MTV modo bora wa mwaka na kuanzia hapo akawa na mwendo wa mafanikio bila kurudi nyuma

.

Media za kimataifa na fashion/modeling industry wanamtaja Alek Wek kwa kuleta mabadiliko makubwa yaliyochochewa na muonekano wake na kujiamini kwingi ambapo licha ya baadhi watu kumponda Kabla kwa muonekano wake, Lakini mafanikio yake makubwa katika high fashion industry ulimwenguni yalichochea wanamitindo wengi weusi kuingia kwenye modelling na pia wanawake wengi weusi kujikubali bila kujibadilisha ngozi zao wawe weupe

.

Oprah Winfrey(63) alikiri hilo pia kwa kusema Kama wakati akikua angebahatika kumuona Alek Wek kwenye majarida basi hata mtazamo wake jinsi alivyokuwa akijichukulia ungebadilika

.

“if (Alek) had been on the cover of a magazine when I was growing up, I would have had a different concept of who I was.” Amesema Oprah

.

Nae Lupita Nyong’o(34) alisema wakati akikua alikuwa mwenye simanzi na kutokujiamini kwa muonekano wake sababu ya baadhi ya watu kumkebehi, Lakini alipomuona Alek Wek kwenye TV akitamba kimataifa mtazamo wake kuhusu yeye na urembo ukabadilika akaanza kujikbali .

“When I saw Alek, I inadvertently saw a reflection of myself that I could not deny, Now, I had a spring in my step because I felt more seen, more appreciated by the far-away gatekeepers of beauty” alisema Lupita

.

Alek asili yake ni Sudan kabila ya Dinka, walikimbia vita na kuingia Uingereza ambapo alianzia modeling huko Lakini kwasasa anaishi nchini Marekani akiwa bado anafanya vizuri

Advertisements
%d bloggers like this: