Skip to content
Advertisements

Paundi milioni 35 kumpeleka Ozil Manchester.

Klabu ya Manchester United imtenga kitita cha paundi milioni 35 kwaajili ya kumg’oa kiungo wa Arsenal Mesut Ozil mwezi huu wa Januari kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

United inaamini kitita hicho kinatosha sana kumg’oa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 raia wa Ujerumani.

Ozil yupo kwenye mwaka wake wa mwisho na amegoma kuongeza mkataba mpya klabuni Arsenal, gazeti la Mirror limesema kwamba Mourinho amepewa ruksa ya kuzungumza na nyota huyo.

Gazeti hilo pia limesema kwamba Mourinho amepanga kutumia paundi milioni 80 kwa mwezi huu wa Januari, na anajiandaa kujidiliana na Gunners kuhusu bei ya kulipa kwa ajili ya nyota huyo

Wenger ana nia ya kumbakiza nyota huyo wa Ujerumani, licha ya Ozili kubakiza siku chache kwenye mkataba wake.

Advertisements
%d bloggers like this: