Skip to content
Advertisements

UTAFITI: KANSA YA MATATITI VITAMIN D NDIYO KINGA KUBWA

Vitamin D, ambayo kwa kiasi kikubwa hupatikana kwa ngozi kupata mwanga wa jua, ina faida nyingi muhimu za kiafya mwilini na utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa vitamin hiyo ndiyo msingi mkubwa wa kuzuia magonjwa mbalimbali mwilini.

Utafiti huo umebaini kuwa vitamin D ni muhimu kwa sababu kiasia cha asilimia 10 ya vinasaba (genes) vya mwili wa binadamu vinaitegemea vitamin hii kufanya kazi yake, kikiwemo kinasaba kinachohusika na uzuiaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na yale ya uvimbe.

Katika utafiti huo ambao pia umeelezewa kwa kina na Dr Mercola wa nchini Marekani katika mtandao wake, imeoneshwa kwamba ukiwa na Vitamin D ya kutosha mwilini, Kolestrol mbaya hushuka na pia huongeza mara mbili uwezo wa mwili kujikinga na saratani ya matiti.

Vilevile utafiti huo umebainisha na kugundua kwamba, kuna uhusiano mkubwa kati ya upungufu wa Vitamin D mwilini na watoto taahira. Ugunduzi huu ni muhimu sana, hasa kwa akina mama waja wazito, kwani madhara ya kuwa na upungufu mkubwa wa Vitamin D unaweza kusababisha kuzaa mtoto mwenye utindio wa ubongo.
Katika makala yake, Dk. Mercola ameeleza kuwa tangu miaka ya 2000, utafiti kuhusu umuhimu wa Vitamin D umeongezeka sana. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2012, tayari zilikuwa zimeshachapishwa tafiti karibu 34,000 na kuna kumbukumbu (references) za kitabibu zaidi ya 800 ambazo zinaonesha uwezo wa Vitamin D katika kuzia saratani.

Kwa mujibu wa mwanzilishi wa mtandao ujulikanao kama GrassrootsHealth, Bw. Carole Baggerly, kiasi cha asilimia 90 ya saratani ya kawaida ya matiti ina uhusiano mkubwa na upungufu wa Vitamin D mwilini.

Katika jarida la ‘Anticancer Research1’, toleo la Machi mwaka huu, kumechapishwa utafiti wa wagonjwa wa kansa ya matiti waliopimwa kiwango cha Vitamin D. Iligundulika kwamba wenye kiasi kingi cha Vitamin D wana uwezekano wa kupona na kuishi kwa muda mrefu mara mbili ya wale wenye kiwango cha chini cha Vitamin hiyo.
VITAMIN D UNAIPATAJE?

Kama nilivyo dokeza kidogo hapo juu, chanzo kikubwa cha Vitamin D ni mwanga wa juu. Utaweza kupata Vitamin D kwa kuota jua, hasa lile la kati ya saa moja asubuhi na saa sita mchana, hata kwa muda wa angalau dakika kumi tu.

Chanzo kingine ni kutumia vidonge vya virutubisho vya Vitamin D vinavyotengenezwa na makampuni yanayoaminika kimataifa.

Hivyo wito wangu kwako msomaji, hakikisha unapigwa na mwanga wa jua kila siku japo kwa dakika chache ili kupata Vitamini hii muhimu kwa kinga ya mwili wako dhidi ya maradhi hatari.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: