Skip to content
Advertisements

Waombolezaji Watimua Mbio Baada ya Mtu Aliyedhaniwa Amekufa Kuibukia Msibani

Wakazi wa kijiji cha Marindi huko Kaunti ya Migori walipaniki na kuchanganyikiwa baada mwanaume wa miaka 35 ambaye aliaminika kuwa amefariki kuibukia msibani nyumbani kwake ghafla
Familia ya mwanaume huyo walikuwa wakimalizia mipango ya mazishi ndipo Okelo Nyamwaga alipojitokeza
Kufika kwake huko kusikotarajiwa kulileta hofu na furaha katika familia yake na marafiki na waombolezaji wengine kukimbia
Nyamwaga alikuwa amepotea kwa miezi miwili na familia yake ilipoteza matumaini ya kumpata akiwa hai
Wiki moja iliyopita marafiki wa Nyamwanga walisema mwili wake ukiwa umeharibika ulikuwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Migori
Mwili huo uliokotwa mtoni ukiwa umeharibika na kupelekwa mochwari

Advertisements
%d bloggers like this: