Skip to content
Advertisements

KENYA: KIONGOZI WA NRN ASAFIRISHWA KWENDA CANADA

KENYA: Serikali imemsafirisha Mmoja wa Viongozi wa NRM, Miguna Miguna kuelekea nchini Canada ikiwa ni saa chache baada ya Majaji kusimamisha kesi zake zote kufuatia Polisi kushindwa kumfikisha Mahakama Kuu

Ifahamike kuwa Miguna Miguna ana uraia wa Kenya na Canada

Taarifa zisizo rasmi zinasema Serikali ya Canada iliiandikia barua Kenya kuonyesha wasiwasi juu ya raia wake alikuwa akinyanyaswa na walitaka arudishwe nchini humo

Hatua hiyo ya Majaji wa Mahakama Kuu inakuja baada ya Kiongozi huyo kufunguliwa kesi ya uhaini kwenye Mahakama ya Kajiado hapo jana

Tarehe 5/02/2018 Mahakama Kuu iliamuru Miguna afikishwe Mahakamani hapo ila Polisi hawakufanya hivyo, kupelekea IG na DCI kuitwa Mahakamani hapo kutolea ufafanuzi swala hilo

Miguna Miguna alikamatwa nyumbani kwake huko Runda kutokana na kushiriki kwake kuapishwa kwa kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga

Advertisements
%d bloggers like this: