Skip to content
Advertisements

Chanzo cha Ugomvi kati ya WCB NA CLOUDS

Yasemekana Tukio lililofanywa na kipindi cha Shilawadu la kujifanya wamepigwa na Mose Iyobo na kwenda kumshitaki Polisi..ndilo lililosababisha yote haya kutokea ,kwa mujibu wa wcb wanasema shilawadu walipika story na wala hawakupigwa na hivyo wamewachafua kwa makusudi.

Pia kwa siku za hivi karibuni nyimbo za WCB zimekuwa hazipigwi Clouds.

Pia kitendo cha RC MAKONDA kuwa mlezi wao wakati Ruge na Makonda hawaelewani hiyo nayo imechangia katika kusababisha mahusiano yao na Clouds kulegalega.

Uanzishwaji wa Wasafi Fm na Wasafi Tv pia yasemekana imechangia kwa kiasi kikubwa katika kufanya mahusiano ya WCB na Clouds kulegalega kwa kiasi kikubwa.

Hakuna kauli yeyote iliyotoka clouds kuhusiana na tukio hili.

Advertisements
%d bloggers like this: