Skip to content
Advertisements

Quavo wa Migos matatani asakwa na polisi wa New York

Msanii kutoka kundi la migos Quavo.

Ripoti zinasema kuwa Idara ya polisi mjini New York ‘NYPD’ ina ushahidi wa kutosha kumkamata Rapa Quavo.

Wiki kadhaa nyuma, Quavo ambaye ni memba wa kundi la Hip Hop la Migos, aliingia kwenye ugomvi na Sonara mmoja anayefahamika kwa jina ‘Eric The Jeweler’, ilikuwa ni siku baada ya Tuzo za Grammy. Kisa kilikuwa Quavo kushindwa kukamilisha malipo ya kazi aliyowahi kumfanyia.

Eric alimfata Quavo kwenye Club moja ya usiku akimtaka ampatie pesa yake kiasi cha $10k, Quavo hakukubali. Kilichofata ni rapa huyo na wenzake waliamua kumshushia kipigo kisha kumwibia Cheni yake yenye thamani ya $30,000.

Sasa kwa mujibu wa TMZ, Idara ya Polisi NY imempigia simu Mwanasheria wa Quavo Drew Findling na kumwambia wana ushahidi wote kumkamata Quavo.

Hata hivyo Findling amepinga vikali tuhuma hizo huku akisema kuwa polisi na Mahakama zinaendeleza Uonevu kwa watu weusi, akitolea mfano wa sakata la Meek Mill
“This is yet another example of a young African – American hip hop star potentially being treated unfairly by the criminal justice system.”- alisema Findling.

credit.InfoHDNews

Advertisements
%d bloggers like this: