Skip to content
Advertisements

Mfahamu Leleti Khumalo,(Sarafina)

Wengi wanamfahamu kwa umahiri wake aliouonyesha kwenye filamu ya sarafina akiwa na umri wa miaka 15 tu, filamu ambayo ilitikisa karibu Afrika nzima na baadhi ya nchi za ugahibuni.

Lakini jina lake halisi ni Leleti Khumalo, muigizaji na sasa ni mtangazaji wa radio, pia ni mwana harakati wa haki za binadamu.

Katika maisha yake baada ya kuwa maarufu alipitia changamoto nyingi kama kuolewa na mwanaume ambaye alikuwa akimtesa.

Mwaka 2016 star huyo aliamua kuweka wazi juu ya ugonjwa unaomsumbua, ambao unaathiri kiasi kikubwa cha ngozi yake,unaojulikana kama ‘Vitiligo’. Moja ya chombo cha habari cha Afrika Kusini kilimnukuu akisema kuwa “imechukua muonekano wangu lakini niko sawa, sitaki maisha yangu yawe kuhusiana na hali niliyonayo, kwani bado mimi ni yule yule muigizaji, mama na mke”. Akisimulia zaidi kuhusu hali hiyo, leleti amesema alijigundua akiwa na miaka 24, mwanzoni alikuwa na hofu huenda mume wake angeacha kumpenda lakini baadaye alijikubali, na kuamua kufurahia maisha yake.

VITILIGO ni Ugonjwa usio na Tiba

Advertisements
%d bloggers like this: