Skip to content
Advertisements

Kambi ya Nick Minaj wafunguka “yupo studio anandaa albamu yake”

Licha ya picha zake kuonekana jana kwenye ujio mpya wa jarida la Vogue kwa mwaka 2018, Nicki Minaj bado amekuwa kimya hasa kwenye mitandao ya kijamii. Ila leo kambi yake imetuambia alipo!

NickiMinaj hana ujauzito, hajapotea wala kujificha, bali amejifungia studio kuitengeneza album yake mpya ambayo imetajwa kuwa kali sana.

Chanzo cha karibu na rapa huyo kimesema, Minaj aliamua kukaa mbali na Insta/Twitter kwa lengo la kuweka akili yake yote kwenye maandalizi ya album hiyo. Unaambiwa anakesha usiku na mchana huku akipewa kampani na Watayarishaji pamoja na swahiba wake, rapa Lil Wayne na Mack Maine na wasanii wengine wa Young Money.

Mpaka sasa tayari baadhi ya nyimbo zimekamilika, na ni kali sana, album inatarajiwa kuachiwa baadae mwaka huu. Kilieleza chanzo hicho.

Advertisements
%d bloggers like this: