Skip to content
Advertisements

Polisi aliyemkamata Meek mill ahusishwa na Ubaguzi/Upendeleo na uonevu.

Polisi aliyemkamata Meek mill ahusishwa na Ubaguzi/Upendeleo na uonevu.

Polisi aliyemkamata Meek Mill mwaka 2007 ndio chanzo cha matatizo yote!

Timu ya Wanasheria wa Meek Mill inaendelea na harakati za kumweka huru rapa huyo, na sasa imegundulika kuwa Polisi aliyewahi kumkamata hapo awali, yupo kwenye list ya (Mwanasheria Mkuu wa Wilaya) ya polisi ambao wamekuwa wakiidanganya mahakama kwa kutengeneza matukio likiwemo hili la Meek Mill.

Katika list hiyo ya polisi ambao wana historia ya kusema uongo, ubaguzi na upendeleo kwa watu, yupo pia Bwana Reginald V. Graham ambaye alimkamata MeekMill mwaka 2007 kwa kosa la kukutwa na silaha pamoja na dawa za kulevya, na aliisimamia kesi hiyo Mahakamani.

Mwishoni mwa mwaka jana, Meek Mill alihukumiwa kwenda jela miaka 2-4 kwa kuvunja masharti ya probation ambayo kesi yake ni hiyo tajwa hapo juu.

Baada ya kugundua madhaifu yake… Sasa Wanasheria wa Meek Mill wamepata mahali pa kuanzia. Ikumbukwe Meek Mill aliwahi kukana mashtaka yote ya kukutwa na silaha kama yalivyoelezwa na Graham ambaye baadae alidai kuwa Meek Mill alimtishia kumpiga risasi hivyo kuzidi kuikuza kesi hiyo.

Kingine kibaya zaidi ni chuki ya polisi dhidi ya rapa huyo mzaliwa wa Philadelphia, ambapo kwenye maelezo yake ya mwaka 2008, Meek Mill alisema polisi Wanne walikuja nyumbani kwake na kumkuta nje, walimtia pingu na kumuingiza ndani kisha kuanza kumpa kipigo kikali. Kama utaona kwenye picha yake (mugshot) Meek Mill akiwa na majeraha pamoja na Plasta usoni.

Advertisements
%d bloggers like this: