Skip to content
Advertisements

‘Greatest Hits’ ya B.I.G yagonga platinum

Kwa mujibu wa Billboard, Album ya nguli wa Hip Hop duniani Marehemu B.I.G. ‘Greatest Hits’ imefikisha mauzo ya nakala Milioni 1, hivyo kupewa hadhi ya Platinum.

Pia katika Chart za Billboard 200, album hiyo imechumpa kutoka nafasi ya 158 hadi nafasi ya 75. Sababu kuu inayotajwa kuchochea mauzo hayo ni kushushwa kwa bei ya ununuzi kwenye mtandao wa iTunes hadi kufikia $4.99 wiki hii.

Album hiyo ilitoka March 6 2007 ikiwa ni mchanganyiko wa nyimbo zake kali kuwahi kuzifanya. Na ilitolewa na studio za Bad Boy pamoja na Atlantic Records kwa lengo la kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo chake.

Greatest Hits ilibeba ngoma 18, zikiwemo: Juicy, Big Poppa, Hypnotize, Dead Wrong, Who Shot Ya na zingine kali.

Album hiyo imemfanya B.I.G. kufikisha Platinum 5 kwenye store ya album zake ikiwemo: Life After Death, Ready To Die, Born Again na Duets.

Advertisements
%d bloggers like this: