Skip to content
Advertisements

Nikki wa pili “Afunguka kuhusu kolabo yao na Bella”

Rapa Nikki wa Pili amesema wimbo ambao ulivuja 2017 wa weusi “Nijue” waliomshirikisha mkali wa muziki wa dansi Christian Bella, upo tayari kuachiwa baada ya kuurudia,

“Awali wimbo huu ulitoka kimakosa na ndio maana hukusikia verse yangu (Nikki), Tulichokifanya ni kuurudia kila kitu na tayari tunayo video mkononi tunategemea kati ya wiki hii tutaiachia” alikiambia kipindi cha Top Hitz cha Dream Fm – Mbeya kinachoongozwa na Mtangazaji Ergon Elly.

Kuhusu hatua waliyofikia kabla ya kuachia albam yao (weusi) nikki wa pili amesema Rapa Joh Makini yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na kampuni ya Max Burudani ambayo itahusika katika kuziuza albam zao (Joh Makini, G Nako, Nikki wa pili pamoja na ile ya kampuni yaani Weusi)

Rapa Nikki wa Pili sasa hivi anafanya vizuri na wimbo wake “Hesabu” aliowshirikisha Joh Makini na muandaaji wa muziki kutoka switch records s2kizy.

Advertisements
%d bloggers like this: