Skip to content
Advertisements

Davido na “THE 30 BILLION TOUR

Ikiwa ni masaa machache yamepita tokea apate mauzo ya juu kupitia ngoma yake ya ‘IF’ na ‘Fall’ hatimaye hit maker wa ngoma hizo amethibitisha kurejesha tamasha la muziki la 30 Billion katika bara la Afrika liitwalo ‘The 30 billion African Tour’

The 30 Billion African Tour inatarajiwa kutimua vumbi Mwezi Machi tarehe 03, mwaka huu katika mji wa Kigali nchini Rwanda katika uwanja wa Amahoro na itafikia tamati Machi 24 katika mji wa Dakar.

Davido ametoa rai hiyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuandika

“The 30 billion African Tour Starts Next month!! What countries will you be attending ??30billionafricatour !! WE NOT STOPPING! NEW MUSIC COMING TOO .”

The 30 Billion World Tour kwa mwaka 2017 ilanza Juni 23 katika mji wa Kiev nchini Ukraine na likahitimishwa nchini Guinea, Septemba 16 2017 ambapo ilihusisha baadhi ya nchi za bara la Afrika, Ulaya na Marekani.

Advertisements
%d bloggers like this: