Skip to content
Advertisements

Maneno ya Mkuu wa Wilaya “akimpongeza Mumewe kwa Kuoa Mke wa Pili.”

Leo February 21, 2018 moja ya stori inayoshika headlines katika mitandao ya kijamii Tanzania ni kumhusu Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah, ambaye amewashangaza watu wengi baada ya kutoa pongezi kwa Mume wake baada ya kuoa mke wa Pili, kwani ni adimu kwa Mwanamke kumpongeza Mumewe kwa kuongeza mke.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram DC Zainabu ameandika kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.

Assalaam Alaykum, Nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu @vanmohamed kwa kuongeza Mke wa Pili. Kwa kuwa dini yetu ya kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi. Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu @only_chibeb wa kusaidiana nae majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa rizki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah. Karibu sana kwenye familia @only_chibeb nimekupokea kwa mikono miwili na inshaaAllah M/Mungu atupe maskilizano na tuishi na mume wetu kwa wema till Jannah InshaaAllah. Baaraka llahu lakumaa, wabaraka alaykumaa, wajamaa baynakumaa fil khaeyr❤️❤️🙏🏼

A post shared by Zainab Abdallah (@zainababdallah93) on

Advertisements
%d bloggers like this: