Skip to content
Advertisements

“Trump Hana Akili “-Cardi B

Shambulio la silaha lilitokea kwenye shule moja mjini Florida wiki iliyopita, lilipata kuzishika headlines za vyombo vingi vya habari duniani.

Tukio hilo lilimlazimisha Rais wa Marekani Donald Trump kulivalia njuga kwa kukaa na wazazi pamoja na majeruhi wa tukio hilo kujadili namna ya kupambana na vitendo hivyo vya kikatili.

Trump alifikia tamati kwa kuja na pendekezo la Walimu kupewa silaha na kuingia nazo shuleni, kama nyenzo ya kujilinda na kuongeza usalama.

Sasa Rapa mtata Cardi B ameibuka na kumtupia za uso Rais Trump, kupitia IG yake, CardiB alipost Meme iliyoambatana na maneno yasiyokubaliana na uamuzi huo wa Rais wake.

Cardi B alimuita Trump mtu asiye na akili, na anafikiria nini kwa walimu ambao wanaingiza mshahara kiasi cha $40,000k kwa mwaka? Marekani itakuwa kiburudisho kwa nchi nyingine.

“Imagine [an] old ass female teacher bussing a burner 🙄This man really out his mind. America must be entertainment to other countries,” – aliandika Cardi B.

Advertisements
%d bloggers like this: