Skip to content
Advertisements

“Belle 9 Atemana na uongozi wake?” Hili hapa jibu lake

Belle 9 amesema ndani ya kipindi kifupi tu ataweka wazi juu ya kutemana na uongozi wake uliokuwa ukimsimamia.

Siku za hivi karibuni kuna minong’ono ya chini kwa chini imekuwa ikiendelea kuwa staa kutoka mji kasoro maji ya blue Morogoro, Belle 9 kuwa hafanyikazi na uongozi wake.

Top Hits ya Dream Fm – Mbeya kupitia mtangazaji wake Ergon Elly ilimtafuta kujua ukweli wa ishu hii… ndipo staa huyo akafunguka,
“kwasasa siwezi weka wazi kwani mimi sio msemaji wa hili ila soon kuna msemaji wa hili ataliweka wazi na watanzania watajua ukweli” alisema Belle 9

Kuhusu kuchelewa kwa albam yake aliyokuwa ameahidi tangu mwala jana (2017) Belle amesema,
“kama ambavyo umesema suala langu na uongozi kuvunjika kwahiyo kuna vitu vilinifanya nichelewe likiwemo hilo na suala la kubariki ndoa yangu ila ipo na itatoka”

Advertisements
%d bloggers like this: