Skip to content
Advertisements

S2kizzy “Ajipanga kuitambulisha record label yake”

Mtayarishaji na Muimbaji wa muziki kutokea katika studio za Switch Records, S2kizzy amesema kuwa kabla ya mwaka kuisha lazima aitambulishe Record label yake.

“Unajua napenda kutoa fursa pia kwa vijana wenzangu wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu ili ku-push muziki wetu kwenda mbali zaidi, sasa kabla ya mwaka huu kuisha nitaitambulisha Record label yangu” alisema S2kizzy alipokiambia kipindi cha Top Hits cha Dream Fm kinachoongozwa na Mtangazaji Ergon Elly.

New Vibe Gang (NVG) ndilo jina la Record Label hiyo ambayo hajaweka wazi itajumuisha wasanii wangapi na jinsia gani.

S2kizzy kwasasa amekuwa akisikika kwenye baadhi ya ngoma kama msanii wa kushirikishwa ikiwemo “Tosamaganga ya Switcher Baba, Hesabu ya rapa Nikki wa Pili.

Advertisements
%d bloggers like this: