Skip to content
Advertisements

Ben pol “Ukizingua kwenye wimbo wake anafanya hivi”

Imekuwa kawaida kwa wasanii kuwaondoa (kufuta lines) waliowashirikisha kwenye wimbo/nyimbo pindi mtu akifanya chini ya kiwango, lakini hii ni tofauti kwa star wa RnB Bongo “Ben Pol” kwani yeye amekuwa hatoi kabisa nyimbo ambazo collabo zake zimefanyika chini ya kiwango.

“Mmmmh!! Mimi sijawahi kumfuta msanii yeyote kwenye collabo zangu bali nimekua nikighairi kabisa kutoa kazi za mtindo huo na hata wyse nilimwambia akifanya chini ya matarajio yangu basi nisingelitoa wimbo huu “Bado Kidogo” – alisema ben pol kupitia Top Hits ya Dream Fm.

Pia masuala ya kufutiana sauti kwenye collabo imewahi kuhusishwa kwenye kile kinachosemekana ndicho chanzo cha ugomvi kati ya star Diamond platnumz na Alikiba.

Star huyu (Ben pol) anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake uitwao bado kidogo aliomshirikisha msanii wake wyse.

Advertisements
%d bloggers like this: