Skip to content
Advertisements

Fahamu;Begi Linalotembea Lenyewe Au (Travel Mate) Kumfuata Mmiliki Wake

Sote tunajua taabu inayopatikana ya ubebaji Begi au mabegi pale tunaposafiri kuelekea katika kituo aidha cha Mabasi, Treni au Ndege.

Adha hiyo sasa ilisha ndoka kabisa baada ya kufanyika mageuzi makubwa ya kiteknolojia kwa kuundwa begi la kisasa.

Travelmate ndio begi la kwanza duniani ambalo linatembea lenyewe bila kubebwa kuelekea kule ambapo muhusika wa begi anapoelekea.

Begi hilo la aina yake linalofanya safari iwe rahisi lilizinduliwa na Travemate mwaka 2016 .

Ni begi linalotumia Teknolojia ambayo hutakuwa na kazi ya kulibeba bali litakuwa linakufuata popote uendapo.

Ili liweze kufanya kazi vizuri na kumfuata mwenye begi limeunganishwa na simu kupitia GPS ili kuweza kumfatilia mmiliki wake kwa usahihi zaidi. Popote utakapoliweka utaweza kulifuatilia
kupitia GPS.

Begi hilo linaweza kutembea kwa vertically (wima) na horizontally (usawa) na unaweza kuongeza mzigo juu yake na likaendelea kutembea bila ya taabu yoyote.

Pia Linaweza kupita popote bila shida yoyote. Linarekebisha mwendo wake ili liwe nyuma yako kidogo. Kasi yake ni maili 6.75 kwa saa (sawa na 10.8km kwa saa) Begi hilo linatumia Battery ambalo unaweza kulitoa.

Unaweza kulichaji kwa njia ya wireless au kwa njia USB. Battery yake inakaa na Chaji kwa muda wa masaa 4 likiwa linatumika. Na bila ya kutumika chaji inakaa kwa muda masaa 100. Pia unaweza kuweka LOCK kwa kutumia fingerprint.
Begi hilo linalozalishwa Marekani linapatikana kwa rangi mbalimbali, na Bei yake linaanzia dola 399 ambayo ni sawa na pesa zetu za madafu kama 850,000/= tsh.
Na begi hilo lilianza kuuzwa mwezi june mwaka 2017 .

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: