Skip to content
Advertisements

Snapchat “Waomba Radhi Ni Baada Ya Kuchochea Ugomvi Kati Ya Chris Brown Na Rihanna”

Mtandao wa kijamii wa Snapchat umewaomba radhi watumiaji wake na watu wote baada ya kuweka tangazo linalo wahusisha Chris Brown na Rihanna huku likionekana kuhamasisha/ kuchochea Ugomvi au Vurugu.

Tangazo hilo la Game liitwalo ‘Would You Rather’ liliwekwa kwa watumiaji wa Marekani pekee, likiwaomba watumiaji wachague ‘Kumchapa kofi Rihanna na Kumpiga Ngumi Chris Brown’.

Tangazo hilo lilitafsiriwa kama uchochezi na kuhamisha Vurugu, hasa ukirudi kwenye tukio la mwaka 2009, ambapo ChrisBrown alimshushia kipigo Ex wake, Rihanna.

Mtandao huo tayari umefuta tangazo hilo na umeomba radhi.

“The advert was reviewed and approved in error, as it violates our advertising guidelines. We immediately removed the ad last weekend, once we became aware. We are sorry that this happened,” – Ulisomeka ujumbe wa Uongozi wa Snapchat.

Tangazo lililowekwa na Snapchat

Advertisements
%d bloggers like this: