Skip to content
Advertisements

UNAJUA KAMA UKIWA NA SMARTPHONE UNAWEZA KUIGEUZA IKAWA COMPUTER?

Ni moja ya mambo ya Ukuaji wa teknolojia, hivyo basi sio mbaya baada ya kukushirikisha ukamshirikisha na mwenzako pia;

  1. Ulishawahi kuhisi kuichoka simu au tablet yako kutokana na udogo wake kwenye kuhifadhi mambo yako? (low storage space)
  2. Muda mwingine inakusumbua na kukwambia memory is full huwezi kuweka kitu chochote

  3. Simu yako imejaa vitu vyako vya muhimu sana na hauna Computer na hautaki kuvifuta na pengine hauna sehemu ya kuvitunza

  4. Ukisoma maelezo vizuri utagundua vingi na utapata njia ya kutatua matatizo mengine mengi pengine hata yakazidi hayo niliyoyataja hapo

Sasa basi ninakupa hii kitu hapa, Kuna Cable Mpya kabisa zinaitwa “OTG Cables“, kirefu cha OTG ni (On The Go) Kwa hiyo kwa kirefu zinaitwa On The Go Cables, Hizi Cable kuna watu hawazifahamu kabisa na hawajui utamu wake. Leo nakudadavulia mambo makubwa utakayoweza kuyafanya endapo una OTG Cable.

CABLE HIZI ZINA PANDE MBILI,

Upande wa kwanza una kichomekeo kama Cha zile chaji za smartphones zetu tulizozizoea, na huu ndio upande unaoingia kwenye simu au tablet na unachomeka kama vile unavyochomeka chaji.

Na upande wa pili wa OTG Cable kuna tundu kubwa la kuchomekea vitu vya asili za USB kama vile flash, lakini kwaupana zaidi naomba nieleze maana kuu ya hili tundu (kwa kitaalamu huwa tunaliita USB Female Port), na linaruhusu kuchomekwa vifaa mbalimbali kwa matumizi tofauti tofauti ila tu vifaa hivyo viwe vya aina ya USB, mfano kama Flashi,Keyboard, External Hard Disk, Speakers n.k.

Sasa basi ukichomeka Cable hiyo kwenye simu au tablet yako kama vile unavyochomeka chaji kwa upande wa kwanza na upande ule wa pili ukachomeka flash, basi utaweza kuisoma kwa ndani ya simu kama vile huwa unasoma memory card yako, tazama picha hapa chini kuelewa zaidi;

Unaweza pia kuchomeka External Hard Disk na ukaitumia kwenye simu au tablet yako, kufanya shughuli mbalimbali kama vile kucheki movies n.k, sijamaliza bado;

Kama simu au tablet yako imejaa vitu unaweza kuvihamishia kwenye flash ukavitunza, kwa mfano hauna Computer, unaweza kununua OTG Cable na flash yako ya 16 GB ukaweka vitu vyako kama Picha, Videos n.k na simu yako ikabaki free na ikawa na spidi ile ile kama ya siku ile ulipoinunua, na hapa hautalalamika tena kuwa simu yako ina uwezo mdogo wa kutunza vitu,.

Kwa wale wanaotamani sana kuwa na Computer lakini hawana uwezo wa kuzinunua, lakini wanamiliki Smart Phones zao nzuri tu, basi hapa nakupa maujanja, nenda dukani ulizia OTG Cable na zinauzwa kwa elfu 5 tu ila kuna sehemu ukienda utapigwa mpaka elfu 40, tembelea duka lolote la simu ulizia.

Ukishanunua OTG Cable, nunua flash zako za 16 GB kama 3 au 5 kama una uwezo, kisha nenda kakopi vitu unavyohitaji kwa mtu mwenye Computer na uviweke kwenye flash yako (mfano flash ya Movies pekee yake, ya madocuments pekee yake, ya miziki pekee yake na ya picha pekee yake,

Najua ugonjwa wetu vijana na wazee kwa mbali ni Miziki, Movies, Kujirekodi Na kupiga Picha hasa kwenye event za kifamilia na hivi vitu hujaza sana simu zetu, hivyo ukiwa na flash zako kama nivyoeleza basi utakuwa salama zaidi, ukiweza hayo basi Ukiwa na simu yako, flash zako, na hiyo OTG Cable ni sawa na kumiliki Laptop.

Utaepuka maswala ya kuhamisha vitu kwa kuchomeka USB cable, au kutumia Bluetooth kuhamishiana vitu vyenye saizi kubwa na vingi kutoka kwenye simu au tablet ya mtu mwingine bali litakuwa ni swala zima la kuchomeka OTG Cable na flash yako kisha unahamisha vitu kwa ku copy na ku paste, na zina spidi nzuri haswaa.

Wale wenye simu kubwa unaweza kuikamilisha simu yako kuwa Computer kwa kuifanya hiyo OTG Cable iweze kuzalisha USB ports nyingine nyingi ili uweze kuchomeka vifaa vingi kwa wakati mmoja kama SPEAKER, KEYBOARD, MOUSE, EXTERNAL HDD n.k.

Advertisements
%d bloggers like this: