Skip to content
Advertisements

Rapper Safaree “amezungumzia busu ambalo Nas alimchapa Nicki Minaj kwenye ‘Right By My side’

Ex wa Nicki Minaj, Rapa Safaree Samuels ameweka wazi hisia zake na kuelezea ilivyokuwa siku ambayo #NickiMinaj alichapwa ‘Kiss’ na Nas kwenye Video ya ‘Right By My Side’ ambayo alishirikishwa pia Chris Brown mwaka 2012.

Akizungumza kupitia Episode ya ‘Easily Offended’ kwenye moja ya Podcast, Safaree alifunguka kuhusu Busu hilo na jinsi lilivyo Muumiza.

“Nilikuwepo siku ya kufanya video ile, Unataka kujua kipi kilitokea? Sikufahamu kama kitendo kile kilitokea mpaka video ilipokuja kutoka.” alisema Safaree.

“Siwezi kudanganya, Niliumia sana kwa kitendo walichofanya. Kabla ya hapo niliwahi kuwa mtu poa tu kwake, nilimpongeza [Nicki] hata baada ya kumkalia Drake mapajani, au kucheza na Lil Wayne, niliona ni upendo tu. Lakini kwa hili la Nas, nilikuwa pale siku nzima lakini sikuona wakati kitendo.

kile kinafanyika. Nikabaki kujilaumu kwamba nilikwenda wapi? nakumbuka nilitoka kama Saa Moja hivi, nafikiri ndio wakafanya ‘Scene’ ile. Bado linaniumiza.”- alimaliza Safaree ambaye penzi lake na Queen huyo wa Hip Hop lilimalizika mwaka 2014.

Advertisements
%d bloggers like this: