Skip to content
Advertisements

Runtown Afikishwa mahakamani Ni baada ya kuvunja masharti ya mkataba

Runtown aburuzwa Mahakamani kwa Makosa ya kuvunja baadhi ya makubaliano ya mkataba wake na lebo ya Eric Many.

Lebo hiyo imeamua kufanya hivyo kwa kile kilichozungumzwa na kuandikwa kwamba, Mwimbaji Runtown amekiuka baadhi ya makubaliano; Moja alienda mjini Las Vegas January 13, 2018 na kuanzia hapo amekuwa akienda kinyume na makubaliano na Uongozi wake.

Kwa mujibu wa maelezo ya Eric Many, Staa huyo wa Nigeria amekuwa akirekodi singles na album bila ridhaa ya lebo yake. Si hivyo tu, pia amekuwa akitumbuiza maeneo mbali mbali na kuchukua viingilio bila ruhusa na ridhaa ya Lebo yake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu namba 4.41 cha mkataba wake.

Advertisements
%d bloggers like this: