Skip to content
Advertisements

Waziri Mwakyembe akasirishwa na kejeri za Diamond kumshambulia Naibu Waziri, Asema maneno haya makali

Waziri wa Habari Sana’a, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na msanii Diamond Platinumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni.

Mwakyembe ameswma @diamondplatnumz ameanza kulewa umaarufu sasa.

Alichokisema Mwakyembe: “Kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, however popular he is.
Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake.

Si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo,” amesema Mwakyembe

Advertisements
%d bloggers like this: