Skip to content
Advertisements

BarakahThePrince awakatisha tamaa mashabiki kuhusu kolabo zake za SautiSol na CassperNyovest

Ulikuwa unahamu ya kuzisikia kolabo za BarakahThePrince alizofanya na #SautiSol na CassperNyovest? Hilo unatakiwa kusahau tena.

Barakaha aliwahi kusema kuwa tayari ameshafanya kolabo kibao na mastaa wakubwa Afrika na kutuhakikishia kuwa ngoma hizo zitapatikana kwenye albamu yake, lakini kwa sasa ameonyesha ni vigumu kuzisikia tena ngoma hizo. ◻

Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ amesema, “Hizo zilikua ni project ambazo zilikuwa under Rockstar kipindi ambacho nilikuwa yao. Ni nyimbo ambazo wanazishikilia wao, walinilipia kila kitu kutoka hapa na kwenda Kenya na kila kitu Production, Producer na kila kitu. Sauti Sol makubaliano yao mikataba. Tulisaini mkataba kabla hatujarekodi, kwa hiyo ilikuwa ni product ya kwao kina Seven.”

“Nimejaribu kuongea nao kupatiwa hizo nyimbo, kulikuwa na ngoma ya Cassper kuna Sauti Sol, wamezing’ang’ania kwa sababu zao wao,” ameongeza

Advertisements
%d bloggers like this: