Skip to content
Advertisements

Chris Brown kwenye msala mwingine mzito wa kumpiga mwanamke

Chris Brown amedakwa na Paparazzi wa TMZ kwenye picha zilizomuonesha akimnyonga shingo mwanamke mmoja.

Picha hizo zilidakwa mjini Miami siku chache zilizopita kwenye moja ya party iliyofanyika kwenye jumba alilokodi Chris Brown. (SWIPE kushoto kuona picha hizo.)

Kwa mujibu wa macho ya watu, imeonekana kama #ChrisBrown alikuwa akimnyonga shingo mwanamke huyo! Lakini kwa nyakati tofauti, Chris Brown na Mwanamke huyo wamefunguka kuwa walikuwa wanacheza.

Mwanasheria wa Breezy, Mark Geragos, ametoa maelezo ya picha hizo na kusema: “Ni rafiki tu, na ni kweli ulikuwa ni mchezo kama alivyothibitisha. Na yeyote aliyevamia faragha yao tutamwajibisha.”- Geragos aliuambia mtandao wa TMZ.

Breezy bado anaandamwa na kovu la kumpiga Rihanna mwaka 2009, kosa lililopelekea kuwekwa chini ya Uangalizi wa Mahakama kwa miaka Mitano.

Advertisements
%d bloggers like this: