Skip to content
Advertisements

Mrisho Mpoto- “Steve Nyerere Punguza Gubu ,wewe umechangia kufa”

Ikiwa zimepita siku tatu toka kutolewa kwa tuzo za sinema za watu zilizofanyika Mlima city ,Wema na Gabo ni baadhi ya wasanii walioibuka kidedea katika tuzo hizo.Kumekuwa na maneno mengi baada baada ya tuzo ikiwemo post ya Uwoya ambayo ilionyesha kumtambua Gabo tu kama mshindi halali.

Lakini siku moja mbele baada ya tuzo msanii mwingine wa maigizo nchini Steve Nyerere aliandika post kwenye mtandao wa Instagram iliyosomeka hivi

“Ntaongea nilicho kiona jana kwenye tuzo ,kwan Ray, JB, Rich, Roams, Aunt Ezekiel, Shamsa Fodi, Duma, Weru, Hemedi, Tausi Mndengela, Mainda, Johari, Uwoya, Marian Ismail, Batuli na wengine wanaofanya vizuri wapo wapi ?Na mbona sijawaona na kuna vijana wasanii chipukizi wanafanya vizuri ,nini tatizo,”

Ikionyeshwa kuwa hakuridhishwa na mwenendo mzima wa utoaji wa tuzo hizo huku akiwataja baadhi ya wasanii ambao anahisi wangefaa kuibika kwenye tuzo hizo.

Mapema leo posti hiyo ya steve Nyerere imeonyesha kutokumpendeza msanii wa Bongofleva Mrisho Mpoto ambaye nae kupitia mtandao wa Instagram aliandika posti iliyosomeka hivi.

“Stive Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele, nikahisi tofauti kidogo: Kwakua kilikua kipindi cha jua kali kidogo….Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na Filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa….ya uigizaji…zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga…siyo lazima apewe unaemtaka wewe Stive. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa.”

Advertisements
%d bloggers like this: