Skip to content
Advertisements

“Nimesikia maneno kwa watu wasioweza hata kuandaa tuzo za kuku” Paul Makonda

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.paul Makonda amewajia juu na kuonyesha kukasilishwa na watu wanaoendelea kuongea kuhusu uhalali wa Wema Sepetu Kuchukua tuzo ya sinema zetu zilizo andaliwa na Azam tv .

Mh.Paul makonda ameposti picha ya mwanadada Wema Sepetu na kuandika caption iliyosomeka.

“Naomba picha uliyopokea tunzo kwasababu nimesikia meneno maneno kwa Watu wasiyoweza kuandaa hata tuzo ya kuku. Hongera Azamu tv 📺 mmefanya zaidi hata ya matarajio ya Watu. Endeleeni kufanya vyema ili mwakani mpokee tuzo tena na wale wenyekukosoa endeleeni kukosoa ili mwakani mkosoe tena. Huu ndiyo utamaduni unaofanya wenyekufanikiwa wachukiwe na wanaowachukia kujifariji kwa maneno bila kuweka bidii ktk kazi”

Hayo ni maneno ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam yiwalenga wale waliokuwa nauponda ushindi wa Wema Sepetu na uandaaji wa tuzo kwa ujumla.

Advertisements
%d bloggers like this: