Skip to content
Advertisements

Unyanyasaji wazidi kumuweka pabaya “Chris Brown”

Wiki iliyopita ilikuwa sio wiki poa kabisa kwa Chris Brown.. Picha zake zenye utata zilizomuonesha akimkaba mwanamke mmoja zimepelekea kwenye matatizo.

Baadhi ya watu mtandaoni (Care 2) wameamua kusaini hati ya pingamizi (Petition) ili kuiondoa Label ya Chris Brown (CBE) kwenye kampuni ya muziki ya Interscope Records kutokana na sababu zake za Unyanyasaji wa Wanawake.

ChrisBrown alianzisha lebo hiyo mwaka 2007 chini ya Kampuni ya Interscope.

Hati hiyo ya pingamizi imeelekezwa kwa CEO wa kampuni hiyo kubwa ya muziki duniani na inasema:

“Brown’s dangerous history of violence against women has gone ignored for too long. Brown is a threat to women and needs to be held accountable for his actions.” tayari watu Elfu 16 wamesaini Petition hiyo ambayo imelenga kufikia saini Elfu 17.

Advertisements
%d bloggers like this: